![]() |
| Baina Mazola (kushoto) akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho kabla ya pambano lao litakalofanyika Dar es Salaam leo. |
MABONDIA Baina Mazola ‘Simba Mazola’ na Fransic Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ leo Jumamosi watatwangana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni katika pambano la raundi nane uzani wa bantam.
Kwa upande bondia mkongwe Miyeyusho amejigamba kuwa atamtwanga mpinzani wake ambaye ananolewa na kocha Cristopher Mzazi .
Mazola akizungumzia pambano hilo alisema anatarajia kumsambaratisha mpinzani wake raundi za mwanzo na kumfanya astaafu ngumi, amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi.
Mratibu pambano hilo Kaizirege Dragon Kaizum amesema maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupimwa uzito kwa mabondi hao.
Mabondia wengine watakaocheza utangulizi ni, Selemani Simba ‘Singida United’ Kutoka Singida dhidi ya Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashid, Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba huku Karim Ramadhani atatwangana na Yohana Dhobian na Keisii Amali atapigana na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani.
Mapambano hayo yatasimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Kocha wa Kimataifa wa Ngumi, Rajab Mhamila amesema atatoa zawadi ya vifaa vya michezo kwa mabondia watakaocheza vizuri, pia kutakuwa na DVD zenye mapambano ya mabondia maarufu waliotamba katika mchezo huo na wanaoendelea kupigana sasa, zinazosaidia kutoa mafunzo ya mchezo wa ngumi na kutambua sheria zake.
Miongoni wa mabodi waliomo kwenye DVD hizo ni, Mike Tyson, Lennox Lewis, anny Pacquiao, Saul ‘canelo’ Alverez ,Floyd Mayweather,Muhamad Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine.

Comments
Post a Comment