![]() |
| Lionel Messi |
MADRID, Hispania
BABA wa mshambuliaji Lionel Messi amefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu mwanaye kuhamia Etihad na kupiga kazi ya soka.
Jorge Messi alikutana na mkurugenzi wa michezo wa City, Txiki Begiristain, ambaye aliwahi kufanya kazi Barcelona hadi mwaka 2012, na kuzungumza kuhusu hatima ya baadaye ya Messi.
Nyota huyo hajasaini mkataba mpya katika msimu ujao atakuwa mchezaji huru kama hataingia mkataba mwingine.
Kuingia mkataba wowote itakuwa ngumu na atalazimika kusubiri hadi majira ya joto mwakani. Messi Jr Julai mwaka huu alifanya makubaliano ya kuongeza mkataba Barca hadi mwaka 2021 ambao haujasainiwa.
Mkataba wake wa sasa unaisha baada ya msimu huu, ikiwa na maana kuwa timu inaweza kumsaini bure mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or .
Barca inaamini kuwa inaweza kuongezea mkataba wa Messi, kwa sasa imekuwa ikisaka mchezaji wa kuziba pengo la Neymar aliyesajiliwa kwa pauni milioni 198 katika timu ya
Paris Saint-Germain ambayo ilivunja mkataba wake wa miaka mitano.
Kwa sasa ili kuvunja mkataba wa Messi timu italazimika kulipa pauni milioni 263 (zaidi ya sh. bilioni 755).
Etihad imekana kwamba haituma ofa yoyote lakini ni ngumu kuuzima uvumi.
City, ambayo juzi ilikamilisha mkataba kwa kuinunua timu ya Girona ambao ni mahasimu wa Barca katika La Liga, msimu huu imetumia pauni milioni 213 (zaidi ya sh. bilioni 611).
Lakini kwa sasa katika dirisha la usajili linaloendelea haiwezi kutumia kiasi kingine cha fedha kinachozidi walichotumia kwa ajili ya Messi, pamoja na mshahara wake.
Baada ya kilio cha mashabiki cha kuondoka kwa Neymar, wakuu wa Barcawasingependa kumuuza Messi haraka.

Comments
Post a Comment