Skip to main content

Mchana nyavu Ghana, Niyonzima wainogesha Simba

Haruna Niyonzima (kulia) baada ya kuwasili Dar es Salaam jana.

KUWASILI kwa kinara  upachikaji mabao katika Ligi Kuu ya Ghana, Nicholas Gyan na  aliyekuwa mchezaji wa Yanga kwa misimu sita mfululizo na nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima kumenogesha usajili wa kikosi cha Simba kwa msimu wa 2017- 2018.

Wawili hao ni wachezani wa mwisho wa kigeni kuwasili kabla ya kufungwa  kwa dirisha la usajili usiku wa  kuamkia leo.

Nyota hao walitua jana  Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) mjini Dar es Salaam na kulakiwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Iddi Kajuna  na viongozi wengine wa klabu, akiwemo Juma Ndambile .




Nicholas Gyan (kushoto) baada ya kuwasili Dar es Salaam , jana.

Wachezaji hao wa kigeni wanaungana na nyota wengine watano na kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe ambaye alijiunga na wanamsimbazi hao msimu uliopita huku akiteuliwa kuwa nhodha katika msimu huu, Juuko Murshid na Emmanuel Okwi wote kutoka Uganda.

Wengine ni James Kotei (Ghana) na Laudit Mavugo kutoka Burundi. Nyota waliokuwa na timu hiyo msimu ulipita na kuachwa kwa kumaliza mikataba ni mlinda mlango Daniel Agyei (Ghana) na mshambuliaji Coast, Frederick Blagnon (Ivory Coast).

Haruna, Gyan na wachezaji wengine wanatarajiwa kutambulishwa rasmi kesho Agosti 8, 2017 katika siku ya Tamasha la Simba (Simba Day) linalofanyika kila mwaka katika tarehe hiyo, hutumika pia kutambulisha jezi na kuwakutanisha mashabiki wa Simba Pamoja kabla ya kauza kwa msimu.

Wachezaji wengine wapya waliosainiwa na timu hiyo ni, John Bocco, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Aishi Manula (wote kutoka Azam), Said Mohamed, Salim Mbonde, Ally Shomary (wote Mtibwa), Emmanuel Mseja, Jamal Mwambeleko (wote Mbao FC), Paul Bukaba ( Atletico Olympic (burundi), Yusuph Mlipili (Toto African).

Siku hiyo ambayo ni hitimisho la Wiki ya Tamasha la Simba Day mbalia ya burudani kitahitimishwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Rwanda, Rayon Sport Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...