![]() |
| Conor McGregor (kushoto) alipokutana na Cristiano Ronaldo. |
BONDIA Conor McGregor anajiandaa kumpiku Cristiano Ronaldo kwa kupata mapato mengi katika orodha ya Jarida la Forbes linaloandika kuhusu mapato na utajiri wa wanamichezo na watu maarufu baada ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lililofanyika Jumapili iliyopita.
Mpiganaji huyo mzaliwa wa Dublin, Scotland anatarajiwa kuingia fedha kiasi cha pauni milioni 77 (zaidi ya sh. bilioni 223) bila ya kujumuisha matangazo ya biashara.
Ronaldo aliongoza kwa kupata mapato mengi mwaka huu aliingiza pauni milioni 71(zaidi ya sh. bilioni 205), anaweza kuzidiwa mapato baada ya McGregor kutwangana na Mayweather kwa raundi 10 mjini Las Vegas na kupigwa kwa TKO, mwamuzi alisimamisha pambano baada ya kuona anazidiwa.
Ronaldo anachezea timu ya Real Madrid na McGregor walikutana mwaka jana na kuzungumza na kutaniana kwa kupigana.
Ronaldo ndiye alimtembelea kambini McGregor ambaye ni bingwa wa ngumi mchanganyiko (UFC) uzani wa light na bondia huyo alimtania kwa kumwambia: Umekuwa namba moja katika orodha ya Forbes, ninapenda kuwa wa 35 au namba nyingine. Nitapanda. Pengine mwaka ujao nitakukuta.' Ronaldo alijibu: 'Sifikiri hivyo.'
McGregor hatakuwa namba moja kwenye orodha ya Forbes ijayo,Mayweather anaweza kuongoza.
Baadhi ya taarifa zinasema Mayweather 'Money' anatarajiwa kupata pauni milioni 233 (zaidi ya sh. bilioni 674.5) kutokana na mapato ya pambano lake la mwishoni mwa wiki mjini Las Vegas.
Lakini mabondia hao wanatarajiwa kuwapita kimapato wananamichezo kama LeBron James, Roger Federer na Lewis Hamilton.
Forbes katika kufanya mchanganuo wa mapato hujumuisha mishahara na bonasi zinazopatikana katika mwaka.

Comments
Post a Comment