![]() |
| Floyd Mayweather (kulia) akimtwanga ngumi Conor McGregor . |
LAS VEGAS, Marekani
BONDIA Conor McGregor amemlaumu refa wa pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather lililofanyika Usiku wa kuamkia Jumapili katika ukumbi wa T-Mobile Arena Las Vegas, Marekani kwa kulimaliza kutokana na kuona amezidiwa na badala yake angemwacha andelea kupigana kwa pamoja na kwamba alikuwa katika hali ya kulewa.
Katika mchezo huo, alishinda kwa TKO kutoka na mwamuzi kusimamisha pambano kumwokoa mpinzani wake huku akipata ushindi wa majaji 2-1 kwa alama 87-83, 89-82 na 89-81.
McGregor alisema:” Kuna mambo mengi kwenye mstari hapa. Refa angenicha mimi niendelee. Nilikuwa nimechoka kidogo.
“Nilikuwa kidogo nimelewa wakati nilipokuwa nimechoka, hivyo ndiyo maana ninafikiria refa angeacha niendelee na kuniacha niangushwe.
“Katika raundi mbili za mwisho angeniacha niende kwenye kona na kukwepa.”
McGregor alikiri kuwa asingeweza kuendelea kwenda sawa na Mayweather (40) ambaye alikuwaakipambana kutaka ashinde ili kuweka rekodi ya kushinda michezo 50 mfululizo.
Alisema: ''Hakuwa na kasi kubwa au kuwa na nguvu zaidi lakini alionesha kucheza vizuri. Ninatakwia kutoa heshima kwa uchezaji wake mzuri wa kipindi chote alichodunu kwenye mchezo,'' alisema na kuongeza alikuwa na furaha kidogo kwa kucheza mchezo huo.
Alisema katika raundi za mwanzo aliona kama alikuwa akimmudu mpinzani wake katika raundi za mwanzo na kuhishi kuwa angeweza kuendelea kipinsi cha katikati hasi mwisho.
Alisema pamoja na kupoteza pambano hilo anafurahi alibeba bendera ya nchi yake (Scotland) iliyokuwa ikimsapoti na kuwa na timu yake.

Comments
Post a Comment