Kylian Mbappe akipasha pamoja na Youri Tielemans asmbaye amejiunga na Monacco akitokea Anderlecht katika majira haya ya joto.
MONACO, Ufaransa
HUKU kukiwa na habari kuwa timu za soka hasimu za Hispania, Real Madrid na Barcelona zinamwania mshambuliaji kinda, Kylian Mbappe, nyota huyo amerejea kwenye timu yake ya Monaco na kuanza mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2017-18.
Barcelona ni timu mpya ambayo imetajwa kuwa kwenye mbio za kuwania saini ya Mbappe, ikiungana na mahasimu wao, Real Madrid .
Nyota huyo mwenye umri wa 18 amekuwa akihusiwa na habari za kutakiwa kwa ada ya pauni milioni 160 (zaidi ya sh. bilioni 472.9) katika majira haya ya joto.
Mbappe alishindwa kung'ara katika mchezo wa kuwania Kombe la Ufaransa ambapo timu yake ya Monaco mabingwa wa Ligue 1 walifungwa mabao 2-1 dhidi ya Paris Saint-Germain.
Mbape alifunga bao ambalo halikukubaliwa kutokana na kuonekana kuotea kabla.
Jana, Mbappe alifanya mazoezi huku akionekana kuwa na ari pamoja na wachezaji wenzie katika uwanja wa La Turbie.
Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, Barcelona imejiunga katika mbio za kutaka kusaini Mbappe, ikitaka azibe pengo la Neymar kama atajiunga na PSG kwa ada ya pauni milioni 196 (zaidi ya sh bilioni 579).
Katika msimu uliopita Mbappe alifunga mabao 26 katika mechi 44 alizochezea Monaco aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ufaransa na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Monaco itacheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1 Ijumaa hii dhidi ya Toulouse .

Comments
Post a Comment