Skip to main content

Mayweather , McGregor waendeleza tambo


Floyd Mayweather (kushoto( na Conor McGregor  walipokutana uso kwa uso  Marekani

LAS VEGAS, Marekani
MABONDIA Floyd Mayweather na bingwa wa UFC light uzani  Conor McGregor wamefanya mkutano mbele ya waandishi wa habari kabla ya pambano lao la jumamosi na kila mmoja amemtambia mwenzie kuwa atamtwanga.

Lakini katika Tambio hizo cha ajabu Conor McGregor  amesema kama ingeruhusisha atumie sanaa mapigano mchanganyiko (ngumi, mieleka, mateke) ambayo amekuwa akipigana mda mrefu angemtwanga kwa haraka zaidi mpinzani wake.

Walifanya mkutano wao jana katika Ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas huku na walionekana kuwa wastaarabu  kidogo lakini vijembe havikukosekana.

Pambano lao litakalofanyika uwanja wa T-Mobile Arena linatajwa litakuwa la malipo makubwa zaidi katika historia ya ngumi, McGregor (29) anatarajiwa kupata dola milioni 100, imeleta uvumi kuwa huenda baada ya pambano hilo linaweza asiendelea kupigana katika taasisi aliyokuwa akipigania.

Pambano hilo litaoneshwa kwa njia ya televisheni katika nchi zaidi ya 220.


Floyd Mayweather (wapili kushoto( r na  Conor McGregor  wakiwa mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani.

McGregor alisema katika pambano hilo anaweza kutumia sekunde 20 na kupata ushindi kisha kufikiria ni bondia gani mwingine atapigana naye.

Mayweather katika mkutano huo hakuonekana hakuonekana kutaka kutukanana na mpinzani wake, kitu ambacho kimetajwa pengine ni kutokana na kapuni za kubeti kuweka kipengele hicho.

Alisema anataka kushinda pambano hilo ili kuwa na rekodi ya kushinda mapambano 50 katika mechi 50 bila ya kupigwa.

"McGregor anaweza kusema anachotaka, pambano likija nitapigana. " Kiakiri, hakuna mwanamichezo aliye imara kama mimi. Nimekuwa katika mchezo huu nikifanya vizuri kwa miaka 21. Nyie mnafikiri kuwa silichukulii pambano hilo kwa uzito? ninalipa uzito,'' alisema

Imeelezwa kuwa mshindi wa pambano hilo atapatiwa mkanda Kutoka Barala za Ngumi la Dunia (WBC) umepewa jina la 'The Money Belt'.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...