Skip to main content

Mayweather amtabiria ushindi McGregor


Floyd Mayweather  (kushoto) alipokuwa akitambiana Conor McGregor.

NEW YORK, Marekani

BONDIA Floyd Mayweather amesema Conor McGregor  ana nafasi kubwa ya kushinda pambano lao linalotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Mayweather ambaye hajapoteza pambano katika mapigano 49 aliyocheza, atatwangana na mpiganaji nyota wa ngumi mchanganyiko zinazohusisha mateke, mieleka McGregory katika Ukumbi wa T-Mobile Arena  mjini Las Vegas, Marekani, pambano linalotajwa kuwa la fedha nyingi zaidi katika historia.

Wawili hao walitukanana na kutoleana vitisho katika miji minne waliyokwenda kutangaza pambano lao, huku karibuni Mayweathe akisema atamtwanga kwa KO, McGregor.

Akizungumza na ESPN, Mayweather  alisema McGregor  ni kijana na ni mrefu zaidi ni mkubwa kuanzia chini hadi juu.

'' Yeye ni kijana sana. Ujana uko upande wake. Nimekuwa nje ya ulingo kwa miaka. Mimi niko katika miaka 40. Kama ukiangalia katika kila gazeti inaonesha Conor McGregor anapewa nafasi,'' alisema.

''Mimi ni mzee, sina kiwango kama nilichokuwa nacho miaka miwili iliyopita. Siko kama nilivyokuwa miaka mitano iliyopita. Nimepoteza hatua.

''Mpiganaji kama Andre Berto hakuwa wa kiwango cha kupigana na Floyd Mayweather, lakini kumbuka nilikuwa na umri wa miaka 38,'' alisema.

Hata hivyo, Mayweather anapewa nafasi ya kushinda pambano hilo baada ya kushinda mapambano yake yote  49. McGregor, hajawahi kupigana chini ya sheria za ngumi.

Mayweather ameadhidi siku ya pambano kucheza mchezo wa kufurahisha natatumi mbinu kama alizotumia katika pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao.

Alisema: '' Mchezo huu hauwezi  kuwa wa kujilinda. Nitakwenda mbele. Ninatajitolea kwa ajili ya mashabiki kwa sababu ya pambano la Pacquiao. Hawakufurahishwa na  uchezaji wangu. Watafurahi safari hii.''

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...