Skip to main content

Mashabiki Simba wamwandalia mapokezi makubwa Niyonzima






Haruna Niyonzima



Mwandishi wetu
WAKATI kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea Dar es Salaam kutokea Afrika Kusini ilikoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kesho kutwa ,mashabiki wanajipanga kufanya mapokezi makubwa ya kiungo wake mpya Haruna Niyonzima.

Niyonzima ambaye ametangazwa rasmi juzi na Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara kuwa sasa ni mchezaji halali  klabu hiyo, yuko  nchini kwao Rwanda baada ya kuomba ruhusa kutatua matatizo yake binafsi, anatarajiwa kuungana na timu yake mpya itakapotoka Afrika Kusini.

Habari ilizonazo Spotifleva mashabiki wengi wa klabu hiyo wanapanga kufanya mapokea makubwa ya Niyonzima ambaye amasjiunga na klabu yao akitokea Yanga aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa kwa misimu sita.

“Tunajipanga kufanya mapokezi makubwa kwa Niyonzima ambaye tunaamini kuwa kwa kushiriana na wachezaji wenzie wataifanyia mambo makubwa timu yetu katika msimu huu,” alisema mwanachama wa klabu hiyo aliyejitambulisha na kwa jina Juma Hussein.

Baada ya kuwasili ataungana na wacheaji wenzie wa Simba ambao watafanya shughuli mbalimbali za kijamii katika wiki ya samba iliyozinduliwa rasmi juzi.

Niyonzima ananatarajiwa kutambulishwa rasmi katika Siku ya Simba Agosti 8  mwaka huu  kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam sanjari na wacheaji wengine wote wa Simba ambapo kutakuwa na mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, pamoja na siku hiyo kupambwa kwa burudani pia jezi mpya zitakaotumia na klabu hiyo zitaoneshwa kwa mashabiki.

Baada ya mchezo wake na Rayon, Simba aitaingia tena kambini kujianda wka mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ukakaofanyika Agosti 23, kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Vodacom Agosti 26, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...