![]() |
| Neymar alipotambulishwa PSG |
BARCELONA, Hispania
MASHABIKI wa timu ya Barcelona wameanza kumwombea dua mbaya wakitaka afe aliyekuwa mchezaji wako, Neymar Santos Jr aliyehamia timu ya Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 198 (zaidi ya sh. bilioni 577.6).
Mashabiki hao walionekana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa dua mbaya kwa Neymar wakati wa mchezo wao dhidi ya timu ya Chapecoense ambayo wachezaji wake 19 walikufa katika ajali ya ndege Novumba mwaka jana.
Wengine walisikika wakitoa maneno ya lugha mabaya kwa mchezaji huyo wakati wa mchezo huo.
Barcelona ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Chapecoense mabao yake yakifungwa na
Lionel Messi, Luis Suarez, Sergio Busquets, Gerard Deulofeu na Denis Suarez.
Kabla ya mchezo huo, mashabiki walishikwa na simanzi baada ya kutambulishwa kwa wachezaji walionusurika Jakson Follman, Neto na Alan Ruschel.
Ruschel alicheza kwa dakika 35, huku wenzie wakishuhudia nje ya uwanja.
Baada ya Neymar kuhamia Paris, ambapo alitoa fedha za kuvunja mkataba wake, katika mchezo huo kulikuwa na mashabiki waliokuwa wakiimba, “Neymar muerete”, ikiwa na maana “ Neymar kufa”.

Comments
Post a Comment