Skip to main content

Madrid yaipiga 3-1 Barcelona


 Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la pili dhidi ya Barcelona.

TIMU ya  Real Madrid imetwaa kombe la Supercopa  la Hispania kwa kuwafunga mahasimu wao Barcelona mabao 3-1.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Camp Nou usiku wa kuamkia leo , mshambuliaji Cristiano Ronaldo aliingia akitokea benchi na kufunga bao la pili kabla ya kutolewa kwa kuoneshwa kadi ya njano ya pili muda mfupi baadaye.

Alipofunga bao wakati wa kushangilia alivua jezi na kubakia kufua wazi, akiwaonesha mashabiki jezi yake yenye namba 7, refa alimwonesha kadi ya njano ya kwanza kwa kitendo hicho, kadi ya pili alioneshwa kwa  kile mwamuzi alichoona kama ni kudanganya kujiangusha katika eneo la penalti la timu pinzani.

Wakati akitoka uwanjani alimsukuma refa kwa kukasirishwa na kadi aliyompatia.

Lionel Messi akitoka uwqanjani kichwa chini baada ya timu ya kufungwa mabao 3-1.

Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane, ilipata bao la kwanza mwanzoni mwa kipindi ya pili lililotokana na Gerard Pique kujifunga lakini Barca ilisawazisha kwa penalti iliyopigwa na Lionel Messi baada ya ya kuonekana kama Luis Suarez alichezewa faulo.

Bao la tatu la  Madrid lilifungwa na Marco Asensio.

Timu hizo zitarudiana tena Jumatano katika Uwanja wa Santiago Bernabeu ikiwa ni mara ya kwanza zinakutana kuwania taji hilo tangu mwaka 2012.

Taji la  Supercopa huwani na timu iliyotwaa ubingwa wa Laliga (Madrid) na ile iliyotwaa Copa de la Ray (Barcelona).

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...