Skip to main content

Madrid, Man Utd kuivuta dunia Super Cup leo




LONDON, Uingereza

TIMU za Real Madrid na Manchester United zitaifanya Dunia kusimama kwa muda leo, wakati zitakapokuwa zikipambana katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa Super Cup).

Kama United itafanikiwa kushinda mchezo huo utakaoanza saa 3:15 mjini Skopje, Macedonia, itakuwa imetwaa taji la nne kwa mwaka huu.

Super Cup huwaniwa na timu iliyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa kwa msimu uliotangulia (Real Madrid) na bingwa wa Ligi ya Europa ( Man United).

United ikiwa chini ya Jose Mourinho ilianza msimu uliopita Agosti, mwaka jana kwa kuifunga Leicester na kutwaa Ngao ya Jamii, kisha ikaifunga Southampton katika fainali ya Kombe la EFL Cup na kuichapa Ajax katika fainali ya Ligi ya Europa.

Kama United itaifunga Real itakuwa ni mara yake ya nne katika historia yake kutwaa makombe manne katika mwaka mmoja.

Mashetani Wekundu hao walishinda mara mbili dhidi ya timu za Hispania kati ya mara 10, ikishinda mara moja kati ya mechi tano zilizochezwa ugenini na nyumbani.

Manchester United ikishinda inaweza kutwaa taji lake la pili la Super Cup baada ya mara ya mwisho kulitwaa 1991 walipoifunga Red Star Belgrade bao 1-0  katika Uwanja wa Old Trafford.

United Inaweza kuwa timu ya pili ya Uingereza kutwaa mara mbili Super Cup, nyuma ya Liverpool iliyotwaa kombe hilo mara tatu.

Kocha Jose Mourinho amepoteza mara mbili katika kuwania taji hilo akiwa kocha, 2013 alipokuwa na  Chelsea mwaka 2003  alipokuwa na FC Porto.

Mourinho anakuwa kocha wa kwanza kuzinoa timu tatu tofauti katika kuwania taji hilo.

Timu za Hispania zimetwaa taji hilo mara saba kati ya nane, timu ya mwisho ikiwa ni Atletico Madrid (2012) walipoifunga Chelsea mabao 4-1, ni timu ya Barcelona na AC Milan pekee zimewahi kutwaa taji hilo mara tano huku Real ikilitwaa mara tatu.

Cristiano Ronaldo ambaye leo atakuwemo kwenye kikosi cha Madrid ameweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 108 katika mashindano yote ya Ulaya ikiwemo mawili katika Super Cup.

United, katika mchezo wa leo itamkosa Eric Bailly na Phil Jones ambao anatumikia adhabu kitu ambacho kitatoa nafasi kwa mchezaji mpya  Victor Lindelof kucheza.

Wachezaji wengine wapya wa United ni wanaoweza kucheza leo ni  Romelu Lukaku na kiungo Nemanja Matic.

Real imewaongeza mchezaji kijana Theo Hernandez na Dani Ceballos  katika kikosi chake ambacho msimu uliopita kilitwaa ubingwa wa Liga Liga na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, wanaweza kuunga na Sergio Ramos katika sehemu ya ulinzi.

United  katika mechi za kujiandaa na msimu iliifunga Real kwa penalti baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa California mwezi uliopita na kushinda mechi tano za maandalizi ya msimu, ikipoteza mchezo mmoja tu kwa Barcelona.

Real, kwa upande wake ilishindwa kushinda mchezo wowote kati ya minne ya kirafiki nchini Marekani katika dakika 90 minutes, ikipoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Barca na kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Manchester City, ushindi wake pekee ulikuwa dhidi ya timu ya MLS All.

Timu zinazotarajiwa kuanza ni 




Je, ni timu gani itaibuka na ushindi katika  mchezo wa leo utakaoanza saa 3:45? Dakika 90 za mchezo zitaamua.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...