![]() |
| Kocha George Lwandamina |
KOCHA wa Yanga, George Lwandamina ameongeza mwaka mmoja kuinoa timu ya Yanga.
Uongozi wa Yanga umemwongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali kumalizika Julai 16, mwaka huu.
Yanga imeshawishika kumwongezea mkataba Lwandamina baada ya kuja na kuwa kocha Msaidizi wa Hans Pluijm kabla kwua kocha mkuu, baada ya Pluijm kupandishwa cheo na kuwa mkurugenzi wa Ufundu kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo, aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kuifanya kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo mara nne mfululizo.
Pia aliifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kutolewa na Mbao FC ya Mwanza.
Boniface Mkwasa, ambaye ni Katibu Mkuu wa Yanga amesema wameamua kumwongezea mkataba Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake.
Mwisho

Comments
Post a Comment