![]() |
| Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza James Milner (wapili kulia) aliyepiga mpira na Havard Nordtveit wa Hoffenheim ya Ujerumani kujifunga. |
TIMU ya Liverpool imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya makundi michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2017-18 baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya Hoffenheim.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na mlinzi wake kinda,Trent Alexander-Arnold (19) kwa mpira wa adhabu, huku bao la pili likipatikana kwa Havard Nordtveit kujifunga alipotaka kuokoa mpira uliopigwa na James Milner.
Bao pekee la Hoffenheim ambayo pia ilikosa penalti kupitia kwa Andrej Kramaric lilifungwa na Mark Uth.
Matokeo ya mechi nyingine:
Qarabag 1-0 FC Cop'hagen
Apoel 2- 0 Slavia Prague
Young Boys 0-1 CSKA Mosc
Sporting 0-0 S Bucuresti
Mechi marudiano zitachezwa Agosti 23, mwaka huu.
Machi za Leo:
Celtic 03:45 Astana
Hapoel Beer-Sheva 03:45 Maribor
Istanbul Buyuksehir 03:45Sevilla
Napoli 03:45 Nice
Olympiakos FC03:45 Rijeka

Comments
Post a Comment