Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Sadio Mane baada ya kuifungia bao timu yao dhidi ya Bayern Munich usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Allianz Arena.
BERLIN, Ujerumani
LIVERPOOL imeendelea kufanya vizuri katika mechi zake za kujiandaa na msimu baada ya kuifunga Bayern Munich mabao
3-0 katika mchezo wa kuwania Kombe la Audi nchini Ujerumani.
Mabao ya kipindi cha kwanza ya Sadio Mane na Mohamed Salah na la kipindi cha pili lililofungwa na Daniel Sturridge yalifanya Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp kupata ushindi mnono katika Uwanja wa Allianz Arena.
Liverpool ingeweza kupata ushindi mnono zaidi kama bao la Adam Lallana lisingekataliwa kwa kuotea.
Bayern inayonolewa na Kocha Carlo Ancelotti imezidi kupata matokeo mabaya katika mechi za kujiandaa na msimu, ilipoteza tatu kati ya nne kwenye Mashindano ya Kombe la Kimataifa kwa kufungwa na Arsenal, AC Milan na Inter katika mchezo wa jana ilicheza vizuri kidogo.
Liverpool kwa ushindi huo itacheza na Atletico Madrid katika fainali, Bayern itapambana na Borussia Dortmund katika mchezo wa kuwania Kombe la DFL-Supercup Jumamosi, pia itacheza dhidi Napoli kuwania nafasi ya tatu.

Comments
Post a Comment