![]() |
| Naby Keita |
LONDON, Uingereza
KLABU ya Livepool msimu huu imeamua kufanya kweli kwa kusaini wachezaji anaoamini wanaweza kuisaidia timu yao kuwa vizuri na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England ambao hawajautwaa kwa za zadi ya miaka 20 na kutaka kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Liverpool inayonolewa na kocha Mjerumani, Jurgen Klopp imekubali kulipa ada ya pauni milioni 60 (zaidi ya Sh. bilioni 174) ambayo itavunja rekodi yake ya usajili kwa kumsaini mchezaji wa Kiafrika, Naby Keita kutoka timu ya RB Leipzig ya Ujerumani.
Nyota huyo raia wa Ghana jana alifanyiwa vipimo England, lakini atabakia na timu ya Leipzig msimu huu kabla ya kujiunga na Liverpool msimu ujao chanzo kimesema.
Liverpool ilikuwa ikimfuatilia nyota huyo anayecheza katika sehemu ya kiungo msimu huu, awali ilituma ofa mbili ambazo zilikataliwa na Leipzig iliyoshika nafasi ya pili katika Bundesliga, ofa ya pili ilikuwa na thamani ya pauni milioni 69.3, alisema mmiliki mwenza wa, Red Bull, Dietrich Mateschitz.
Leipzig ilikuwa ikisema wazi kwamba Keita hauzwi kwa bei yoyote katika majira haya ya joto kwa kuwa klabu inataka kumtumia katika ligi ya ndani na Ligi ya Mabingwa ambayo wanashiriki kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Hata hivyo, mkataba wa Keita una kipengele cha kuuvunja kwa pauni milioni 48 kuanzia Julai Mosi 2018, Liverpool imekubali kulipa fedha hizo pamoja na kiasi kingine ambacho hakijawekwa wazi lakini inadaiwa jumla yake kufikia pauni milioni 60.
Kwa kumsaini mcheaji huyo ina maana imevunja rekodi ya wachezaji wake wengine iliowasaini kwa fedha nyingi, wa mwisho akiwa ni Andy Carroll iliyomsaini kwa pauni milioni 35 (zaidi ya sh. bilioni 10) mwaka 2011 akitokea Newcastle.
Liverpool jana ilithibitisha kuwa imalizana na RB Leipzig na Keita alisema: "Kilichomfuarahisha ni sana ni kuwa sehemu ya mradi wa Liverpool wa kuofanya klabu kuwa imara zaidi.''
Alisema kwa sasa ataendelea kuweka mtazamo na kuwajibika kwa timu yake kwa muda uliosalia ili kufanikisha malengo ya msimu huu, huku akijua ana hatima yake ya baadaye.
Katika majira haya ya joto, Liverpool imewasaini winga Mohamed Salah kutoka Roma kwa pauni milioni 34 (zaidi ya sh bilioni 98.6), mlinzi Andrew Robertson kutoka Hull kwa ada ya pauni milioni 8 (zaidi ya sh. bilioni 23 na mshambuliaji Dominic Solanke kama mchezaji huru akitokea Chelsea alikomaliza mkataba wake.
Miamba hiyo ya Anfield kwa sasa pia inajipanga kumsaini kiungo wa Monaco, Thomas Lemar kwa ada ya pauni milioni 60 ( zaidi ya sh. bilioni 174 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi hii.

Comments
Post a Comment