LONDON, Uingereza
TIMU ya Liverpool imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya usiku wa kuamkia leo kuichapa mabao 4-2 dhidi ya Hoffenheim ya Ujerumani katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo.
Kwa ushindi huo Liverpool imesonga mbele kwa kupata jumla ya mabao 6-3, katika hatu ya makundi sasa imeungana na timu nyingine za England za Chelsea, Manchester City, United na Totteham.
Waliofunga mabao kwa Liverpool ni Emre Can (mawili Can dk10, dk 21; Mo Salah dk18; Firmino dk 63) na Mo Salah dk. 63.
Mabao mawili ya Hoffenheim yalifungwa na Mark Uth na Sandro Wagner.
![]() |
| Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akishangilia. |
Timu 32 zilizofuzu hatua ya makundi zitakazo kuwa za kwanza katika upangaji makundi leo ni Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Chelsea, Shakhtar Donetsk, Monaco, Spartak Moscow.
Zitakazo kuwa chungu cha pili ni Barcelona, Atletico, Paris Saint-Germain, Borussia Dortmund, Sevilla, Man City, FC Porto, Man United.
Chungo cha tatu ni: Napoli, Tottenham, FC Basel, Olympiakos, Anderlecht, Liverpool, Roma, Besiktas.
Chungu cha nne ni: Celtic, CSKA Moscow, Sporting CP, APOEL Nicosia, Feyenoord, NK Maribor, FK Qarabag, RB Leipzig.
Hatua ya makundi inatarajiwa kuanza Septemba 12-13 mwaka huu.


Comments
Post a Comment