Skip to main content

Ligi FDL kuanza kurindima Sept 24





Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia

LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) imepangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu kwa kushirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila moja.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa kwa vyombo vya habari  Dar es Salaam jana, awali ilitangaza makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19.

Kwa mujibu wa makundi hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Ligi ya TFF, Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.

Kundi ‘B’ lina timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.

Kundi ‘C’ linajumuisha timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rhino Rangers ya  Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

Pia, TFF imeagiza timu za Ashanti United, Friends Rangers, KMC na Polisi Dar ya Dar es Salaam kuwasilisha majina ya viwanja vitakavyotumiwa na timu zao wakati wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.

Kutaja viwanja hivyo ni matakwa ya Kanuni ya 6 (1) za kanuni Mama ya VPL inayozungumzia Viwanja kadhalika kusomwa pamoja na Kanuni ya 11 inayozungumzia Leseni za Klabu kwamba kila timu haina budi kuwa na viwanja vya mcehi za nyumbani ikiwa ni masharti ya kupata leseni ya klabu.

Wakati huohuo; TFF) imeandaa semina ya siku moja kwa Madaktari wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayofanyika Ijumaa Agosti 4, mwaka huu kuanzia saa 2.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 73 ya Ligi Kuu, kila klabu ya Ligi Kuu inatakiwa kuwa na daktari wa timu ambaye pamoja na mambo mengine atahakiki afya za wachezaji na viongozi wa timu.

Kila klabu inatakiwa kuhakikisha daktari wake anahudhuria semina hii muhimu itakayoendeshwa na Kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Paul Marealle.

Bodi ya Ligi itagharamia nauli ya basi ya kuja na kurudi Dar es Salaam kwa kila mshiriki.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...