Skip to main content

Kocha Wenger ataka mshikamano Arsenal



LONDON, Uingereza
BAADA ya kuiwezesha Arsenal kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Chelsea kwa mikwaju ya penalti katika mchezo uliopigwa jana, Kocha
Arsene Wenger amewataka mashabiki wa timu hiyo kubakia na mshikamano .

Wenger ambaye katika msimu uliopita alikuwa haungwi mkono na mashabiki wengi wa timu hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao, amesema kuwa ana matumaini msimu huu mambo yatakuwa mazuri.

Pamoja na kutwaa ubingwa wa Kombe la FA Cup mwishoni mwa msimu uliopita, Wenger aliasaini mkataba mwingine, uamuzi ambao uliwaudhi baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Msimu huu.

Katika msimu huu kuna shabiki alivamia uwanja wakati wa mchezo wa kirafiki akitaka kwenda kumtukana, lakini kwa kutwaa ngao ya jamii katika Uwanja wa Wembley itaongeza ari kwa Wenger na timu hiyo.

Arsena ilishinda Chelsea kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya mchezo kuisha kwa sare ya bao 1-1, Wenger mara moja ametaka ushindi huo kuongeza mshikamano kabla ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Ijumaa wiki hii dhidi ya Leicester.

" Nigependa mashabiki kuwa nyuma ya timu kwa kuwa tutapitia vipindi vizuri na visivyokuwa vizuri, tunataka kuungana na kuwa pamoja na katika msimu wote,'' alisema.

Ushindi huo umefanya Wenger kutwaa Ngao ya Jamii mara saba, lakini imetwaa kwa mara ya mwisho baada ya kupita miaka saba.

Arsenal ilianza kufungwa katika mchezo huo dakika ya 46 kwa bao la
Victor Moses, Chelsea ilipata pigo  kutokana na Pedro kuoneshwa kadi nyekundu, katika dakika ya  82 ilisawazisha kupitia kwa Sead Kolasinac.

Katika upigani penalti waliokosa kwa Chelsea ni mlinda mlango, Thibaut Courtois  na mshambuliaji mpya Alvaro Morata huku Olivier Giroud  akifunga penati ya mwisho ya ushindi kwa  Arsenal.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...