JOHANNESBURG, Afrika Kusini
KOCHA wa timu ya Orlando Pirates ambayo jana iliifunga Simba bao 1-0, Kjell Jonevret amejiuzulu.
Pirates imetoa taarifa leo inasomeka: 'Orlando Kocha wa Pirates Football Club , Kjell Jonevret ametoa barua ya kuacha kazi (kujiuzulu).
'Bw. Jonevret amemshukuru mwenyekiti wa Orlando Pirates, Dk. Irvin Khoza, klabu na mashabiki kwa kumpati nafasi ya kuwa kocha wa klabu.'
Jonevret amesema: “Ningependa kuishukuru klabu kwa nafasi niliyopatiwa. Bahati mbaya kazi haikufanyika katika ilivyopangwa. Ninawatakia kheri klabu na mashabiki kwa siku zijazo.”
Mwenyekiti wa Bucs , Irvin Khoza alisema: " Ninamtakia kheri Kjell Jonevretkatika shughuli zake za baadaye."

Comments
Post a Comment