![]() |
| Jugern Klopp (kulia) akitaniana na Pep Guardiola katika moja ya mechi zilizokutanisha timu zao. |
LONDON, Uingereza
JURGEN Klop amesema timu ya Manchester City ni ya kipekee anaipa nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Kocha huyo wa Liverpool naye amemshambulia Pep Guardiola kwa kutumia fedha nyingi kusajili.
Alisema hayo kabla ya Ligi Kuu England kuanza leo, Arsenal ikipambana na Leicester City, Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amesema Pep, kwa kumsaini Gabriel Jesus na wachezaji wengine katika majira haya ya joto imefanya timu yake kuwa imara zaidi.
Wachezaji wengine waliosainiwa na City ni beki Benjamin Mendy, Kyle Walker na Danilo amewaondoa Bernardo Silva na Ederson katika Uwanja wa Etihad walioiingizia timu zaidi ya pauni milioni 26.
Klopp aliiiambia DAZN: “ Timu inayopewa nafasi lazima itakuwa Manchester City. Walicheza soka ya kusisimua msimu uliopita na ilikuwa na matatizo machache. Wao wazi kabisa wana nafasi. Safu yao ya ushambuliaji iliyoundwa na vijana ni nzuri,''
Klopp (50) ambaye timu yake itaanza kampeni ya ligi ugenini Vicarage Road dhidi ya Watford kesho alisema anatumaini msimu huu kumaliza juu kadiri iwezekanavyo.
Pia alisema anatumaini Manchester United itatoa ushindani mkubwa sanjali na Chelsea ambayo haitakwua na Costa lakini imemsajili [Alvaro] Morata na kumpoteza [Nemanja] Matic.

Comments
Post a Comment