| Mashabiki wa Yanga. |
KIWANGO kilichooneshwa na wachezaji wa Yanga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Chipukizi katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kimewakuna mashabiki wa Yanga.
Licha ya kwamba katika mchezo huo Yanga ilipata ushindi mduchu wa bao 1-0.
Ushindi huo umefanya kuweka rekodi ya kushinda mechi zake zote tatu za kirafiki ilichocheza Zanzibar ilikokwenda kuweka kamba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Simba Jumatano hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo mwanzo iliocheza Uwanja wa Amaan , Yanga iliichapa Mlandege mabao 2-0, kabla ya kushinda bao 1-0.
Katika mechi hizo waliofunga mabao ni Ibrahimu Ajibu mawili na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Katika wa jana Gombani bao pekee la Yanga lilifungwa na Haji Mngwali kwa mpira wa adhabu.
Mashabiki wengi walioshuhudia mchezo huo kupitia televisheni walipongeza wachezaji kwa kucheza kwa uelewano mkubwa, kwa kasi na kupasiana huku kiungo mpya wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshisbimbi akicheza mchezo wake wa kwanza na kung'ara kwa pasi murua.
Kutokana na uchezaji mzuri baadhi ya mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameridhishwa ka kiwango na kuwa na matumaini timu yao kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Simba, Jumatano hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga kilichocheza kipindi cha kwanza ni Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Pato Ngonyani, Maka Edward, Pius Buswita, Said Juma ‘Makapu’, Amissi Tambwe/Said Mussa, Matheo Anthony na Juma Mahadhi/Yussuf Mhilu.
Kipindi cha pili; Youthe Rostand, Hassan Kessy/Juma Abdul, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’, Papy Kabamba Tshisbimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu, Emmanuel Martin na Raphael Daudi.
Comments
Post a Comment