Skip to main content

Kipigo cha bao 4-0 chamvuruga Wenger


Kocha wa Arsenal, Arsene  Wenger (kushoto) na benchi lake la ufundi wakiwa wamechanganyikiwa wakati mchezo ukiendelea huku timu yao ikiwa imefungwa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Anfield jana.

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger  amesema hakumbuki ni wakati gani timu hiyo aliyoinoa kwa zaidi ya miaka 20 imewahi kucheza vibaya kana iliyocheza na Liverpool na kupata kipata kipigo cha matendegu ya kitanda (mabao 4-0).

Amewataka mashabiki radhi na kuwaomba kuendelea kuwa pamoja na timu baada ya kipigo cha timu yao alichokiita kama ni janga na udhalilishaji

"Kama kuna watu wanahisi mimi ni tatizo, ninawataka radhi kwamba mimi ni tatizo," Wenger aliiambia Sky Sports.

"Lakini tunataka mashabiki wetu kuwa na sisi hata wakati tunapopoteza kama vile."
Alisema: " Kitu pekee ambacho tunaweza kufanya ni kurejea nyuma kujiandaa na kuja kucheza vizuri."



Katika mchezo huo, uliopigwa uwanja wa Anfield wachezaji wake walionekana kama walikuwa hataki kuwepo uwanjani na kocha kuonekana kama amemepotea njia hajui aende wapi.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal nao wamechanganyikiwa wanajiuliza ni kwanini kocha wao alimwacha katika benchi mchezaji ghari kwenye timu hiyo aliyemsaini msimu huu Alexandre Lacazette ( kwa pauni milioni 53 ambazo nji zaidi ya ya sh. bilioni 152.7)

Kwa kipigo hicho, Arsenal haijashinda dhidi ya Liverpool katika michezo 11, ikifungwa mechi sita na kutoka sare tano, pia haijashinda katika Uwanja wa Anfield kwa miaka mitano. 

Mashabiki wanajiuliza ni kwanini Hector Bellerin alichezeshwa sehemu ya beki wa kushoto wakati anachezea mguu wa kulia huku Sead Kolasinac anayechezea mguu wa kushoto kwa asili alikuwepo?

Liverpool ilicheza kwa uelewano mkubwa na kulinda lango lake, ambalo halikuwa na msukosuko mkubwa.


Mshambuliaji wa Roberto Firmino (katikati) kishangilia baada ya kufunga bao huku akifuatwa na mshambuliaji wenzie Mohammed Salah (kushoto) na Sadio Mane ambao nayo walifunga bao moja kila moja na Daniel Sturridge ambaye hayuko pichani.


Sehemu ya mlinzi wa kati ilipwaya Aaron Ramsey na Granit Xhaka waliruhusishwa kushambulia lakini wakaacha mlango wazi na kuruhusu washambuliaji wa Liverpool kushambulia.

Kwa upande wa Liverpool, ilikuwa na Jordan Henderson na Georginio Wijnaldum  na Emre Can ambao walikuwa wakiwalisha washambuliaji

Roberto Firmino na Sadio Mane walifunga mabao mawili kwa Liverpool kipindi cha kwanza kabla ya  Mohamed Salah na Daniel Sturridge kufunga mengine mawili kipindi cha pili.

Kipigo hicho kimefanya Liverpool kufikisha pointi saba katika mechi tatu na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo huku Arsenal ikipoteza mchezo wa pili katika mechi tatu. Ilishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Leicester City mabao 4-3 kisha ikafungwa bao 1-0.


Mshambuliaji wa  Arsenal, Alexis Sanchez akicheka kwa huzuni wakati timu yake ikicheza uwanjani huku ikiwa imepigwa mabao 4-0.

Katika mechi mbili za mwanzo, Liverpool ilitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Watford, ilishinda bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.

Liverpool: (4-3-3): Karius,Gomez, Matip, Lovren, Moreno, Wijnaldum, Henderson, Can/Grujic, Mane/Sturridge, Firmino/Milner na Salah.

Arsenal: (3-4-3): Cech , Koscielny, Monreal, Oxlade-Chamberlain/ Lacazette, Xhaka , Ramsey/Coquelin, Bellerin, Sanchez/Giroud , Welbeck na Ozil.

Msimamo Ligi Kuu England

Na Timu         P W D L GD PTS

1      Manchester United 3 3 0 0 10 9
2 Liverpool        3 2 1 0 5 7
3 Huddersfield Town 3 2 1 0 4 7
4 Manchester City        3 2 1 0 3 7
5 West Brom Albion 3 2 1 0 2 7
6 Chelsea        3 2 0 1 2 6
7 WatfordWatford        3 1 2 0 2 5
8 Southampton        3 1 2 0 1 5
9 Tottenham Hotspur 3 1 1 1 1 4
10 BurnleyBurnley        3 1 1 1 0 4
11 Stoke City                3 1 1 1 0 4
12 EvertonEverton        3 1 1 1 -1 4
13 Swansea City        3 1 1 1 -2 4
14 Newcastle United 3 1 0 2 0 3
15 Leicester City        3 1 0 2 -1 3
16 ArsenalArsenal        3 1 0 2 -4 3
17 Brighton&Hove Albion 3 0 1 2 -4 1
18 Bournemouth        3 0 0 3 -4 0
19 Crystal Palace        3 0 0 3 -6 0

20 West Ham United 3 0 0 3 -8 0


Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...