![]() |
| Hamis Kilomoni |
KAMATI ya utendaji ya Simba imesimamisha uanachama wa Mzee Hamis Kilomoni na kumuondoa kwenye baraza la wadhamini wa klabu kutokana na kupeleka kesi mahakamani.
Uamuzi huo umetangazwa katika mkutano mkuu wa Simba ulioafanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana na nafasi yake imechukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi.
Kamati hiyo pia, Simba imepanga kumtumia barua Mzee Kilomoni ya kumtaka afute kesi mahakamani na la sivyo atafutwa uanachama moja kwa moja.
Katika mkutano huo Prof. Juma Kapuya amepitishwa kuwa mdhamini wa klabu ya Simba na kuchukua nafasi ya Marehemu Ally Klaiyst Sykes

Comments
Post a Comment