Kanye West (kushoto) na Jay-Z
NEW YORK, Marekani
MASHABIKI wa rapa Kanye West wamekerwa na kitendo cha Shawn Corey Carter, maarufu kama Jay-Z kutoa makala ya filamu inayoeleza na kuonesha safari yake ya muziki na wakiwa pamoja kama marafiki kabla ya kutofautiana na kuwa maadui.
Nyota hao ni wasanii waliouza zaidi kazi zao wakiwa na nyimbo nyingi zilizofanya vizuri na wana mamilioni ya mashabiki.
Baada ya kuangalia makala hiyo iliyopewa jina la
Maadui wa Hadharani 'Public Enemies' – Jay-Z vs Kanye iliyorusha na Channel 4 Jumatatu iliyopita, mashabiki wa Kanye walitumia mtandao wa Twitter kumlaumu rapa wa New York, Jay-Z kwa hatua yake na kusema amemtumia mtu aliyekuwa akimsimamia awali kujikweza kibiashara .
Filamu hiyo iliyopigwa mwaka 2011 imerushwa baada ya nyota hayo waliokuwa rafiki kugeuka maadui na kufanya mashabiki wao kugawanyika.
Baada ya kuonesha uhusiano wao ulivyokuwa katika filamu hiyo, ambapo Jay- Z alikuwa kama mshauri na msimamizi wa msanii mwenzie, mashabiki wa Kanye ambaye ni mzaliwa wa Chicago wameonekana kutofurahia na kumwonea huruma msanii wao.
Filamu hiyo inawaonesha tangu walipokuwa vijana, katika moja ya sehemu anaonekana Eugene McNair (rafiki wa Kanye), akionesha chumba cha kulala cha Kanye ambacho walikuwa wakitumia kurekodi nyimbo pamoja.
Pia alifungua katika sehemu ya kula, ambayo pia ilikuwa na vifaa vya muziki na vipeperushi vya marapa maarufu, Eugene anaonekana akitoa maelezo ni jinsi gani kazi ya kurekodi ilikuwa ikifanyika wakati huo.
'' Tulikwenda kwenye kitanda chake, alikuwa na mambo yote ya kiafrika katika nyumba, kulikuwa na makasha ya kanda za muziki kila mahali, kulikuwa na picha za utupu, alikuwa na nguo mpya.''
Filamu hiyo haielezi jinsi wawili hao walivyofanyikiwa kuwa juu, lakini inaonesha Jay-Z akiwa na mshauri wa aliyemfanya Kanye kuwa juu.
Baadhi ya watazamaji wamesema prodyuza aliyekuwa kugeuka kuwa rapa, Kanye alikuwa na kipaji zaidi kati yao, huku mtazamaji mmoja akiandika kwenye mtandao: 'Kayne na Jay-Z, Jamaa ni jiniasi.'
Tammy Cuff, alisema: 'Ninawapenda wote Jay-Z na Kanye kwa sababu tofauti, lakini College Dropout (albamu ya kwanza ya Kanye) ilikuwa nzuri na
Jay-Z alikuja kama mtu wa kuwatumia.
Shabiki mmoja, alisema kwamba akiwa kama prodyuza, Kanye alimsaidia Jay-Z kutengeneza nyimbo nzuri zilizofanya vema.
Mwingine alisema Jay -Z anamtumia West kwa biashara zake.
Shabiki wa Jay- Z, Chrome Hitz alimtetea nyota wake kwa kusema kuwa bila ya rapa wa New York, Kanye West asingeweza kupanda juu.
Hata hivyo mashabiki wengine baada ya kuangalia filamu hiyo wameifagilia kwamba imeonesha maisha marapa hao walipitia na wengine kusema wao ni alama ya muziki na wana vipaji vikubwa.
Wawili hao walifanya kazi pamoja 2011, albamu yao ya pamoja 'Watch The Throne' ilifanya vizuri na kuuza nakala nyingi duniani.
Wote wawili wameoa, mbali ya muziki wanajihusisha na biashara ya mavazi.
Jay-Z, ana lebo yake ya muziki ya Roc-A-Fella Records , Kanye aliwahi kufanya kazi kwa muda mfupi pamoja naye alipotoka Chicago kwenda New York kutafuta namna ya kutoka.
Baada ya kuacha alifanya muziki kivyake na kuweza kuwa juu katika muziki wa hiphop na kuwa maarufu kama Jay Z.
Albamu nyingine ya Jay-Z inayokuja bado ina alama za vidole vya Kanye ambaye alikuja kuoana na nyota wa runinga, Kim Kardashian.
Kanye kwa sasa haelewani na Jay Z, katika onesho lake alilofanya Sacramento, Marekani alisema amekuwa hampigii simu, anamjua ana watu wanaoweza kupoteza uhai wake (wauaji) lakini asiwatume kumwangamiza.
Pia akiwa jukwaani alimpiga kijembe mke wa Jay-Z, Beyonce kwamba amesikia hafanyi maonesho hadi ashinde tuzo ya video bora ya mwaka na kueleza kuwa hushinda tuzo kwa mipango.
Baada ya kutoa vijembe vyake kwa kutumia kipaza sauti mbele ya mashabiki, Kanye alikitupa jukwaani na kuondoka huku akiwaacha mashabiki wakiwa wamechanganyikiwa.
Kwa wakati huu, Kanye amekuwa akitibiwa ugonjwa wa msongo wa mawazo. Lakini pia kuna habari ameanza kufanya kazi ya kwajili ya kutengeneza albamu yake mpya.
Kwa upande mwingine Jay-Z mwezi uliopita aliachia albamu yake ya 4.44, ambapo kuna wimbo unaonekana kama anaomba radhi kwa Beyonce ambaye hivi karibuni alimzalia watoto pacha kwa kutokuwa mwaminifu kwake.

motaisra Sarah Miller click here
ReplyDeleteunzydeaxdi