![]() |
| Jeff Horn (kulia) na Manny Pacquiao walipotwangana katika pambano lao lililopita. |
Kwa kupoteza pambano hilo , Pacquiao alipoteza mkanda wa WBO uzani wa welter na kusema kuwa atataka kurudiana na mpinzani wake huyo ambaye ni mwalimu wa zamani wa shule.
Horn ambaye ushindi wake ulilalamikiwa na Pacquiao kabla ya Oganaizesheni ya Masumbwi Duniani kuteua majaji watano na kuwataka kulipitia pambano hilo kwa njia ya video kisha kumpata mshindi na matokeo kuonesha Horn alishinda kwa majaji watatu kwa wawili, amethibitisha kurudiwa kwa pambano hilo.
Alisema pambano hilo litafanyika Brisbane, Austarilia mwaka huu.
Pacquiao naye amethibitisha kurudiana na Jeff Horn mjini Brisbane baadaye mwaka huu ,
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika Novemba Uwanja wa Suncorp ambao watu 50,000 walimshuhudia mwalimu wa zamani wa shule, Horn akimshinda kwa pointi Pacquiao kwenye pambano la raundi 12 kuwania taji la WBO uzito wa Welter.

Comments
Post a Comment