Skip to main content

Iniesta, Ronaldo, Messi kuwania Tuzo Mchezaji Bora Fifa

Kutoka kushoto: Lionel Messi,Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) limetoa orodha ya wanasoka 24 ambayo wanaoshindania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka 2017.

Katika orodha hiyo yumo kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta, jina ambalo halikutarajiwa akiwa ameanza kucheza katika mechi za La Liga 13 tu msimu uliopita, tatizo kubwa ikiwa ni umajeruhi.
Mtetezi wa tuzo hiyo Cristiano Ronaldo kama kawaida yumo pamoja na Lionel Messi na wachezaji wawili wa Juventus, Paulo Dybala na Gianluigi Buffon .
wachezaji wa Ligi Kuu England waliojumuishwa ni Alexis Sanchez, N’Golo Kante, Zlatan Ibrahimovic na Eden Hazard.

Katika otodha hiyo wamo wachezaji nyota wa zamani waliojumuishwa ambayo nao mmoja wao atapata tuzo akiwemo Diego Maradona, Cafu, Carles Puyol, Edwin van der Sar na Jay Jay Okocha.

Majina matatu ya mwisho kwa kila kundi yatatajwa kati ya Agosti 21 na Septemba 7 mwaka huu watakahusika kuchafua ni manahodha wa timu, mkocha na wawakilishi wa vyombo vya habari.

Orodha kamili ni kama ifuatavyo;
Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund)
Leonardo Bonucci (AC Milan, Juventus 2016-17)
Gianluigi Buffon (Juventus)Dani Carvajal (Real Madrid)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Paulo Dybala (Juventus)
Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
Eden Hazard (Chelsea)
Zlatan Ibrahimovic (Free agent, Manchester United kwa 2016-17)
Andres Iniesta (Barcelona)
Harry Kane (Tottenham)
N’Golo Kante (Chelsea)
Toni Kroos (Real Madrid)
Robert Lewandowski (Bayern Munich)
Marcelo (Real Madrid)
Lionel Messi (Barcelona)
Luka Modric (Real Madrid)
Keylor Navas (Real Madrid)
Manuel Neuer (Bayern Munich)
Neymar (Paris Saint-Germain, Barcelona kwa 2016-17)
Sergio Ramos (Real Madrid)
Alexis Sanchez (Arsenal)
Luis Suarez (Barcelona)
Arturo Vidal (Bayern Munich)

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...