![]() |
| Zlatan Ibramovic |
LONDON, Uingereza
ZLATAN Ibramovic amekubali kukukatwa mshahara wake wake asilimia 50 ili kubakia katika timu ya Manchester United.
Nyota huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35, atakuwa akilipwa nusu ya pauni 367,000 (zaidi ya sh. bilioni moja) kwa wiki, katika mkataba wake mpya wa mwaka mmoja aliosaini .
Gazeti la SunSport limesema kuwa nyota huyo kwa sasa atakuwa akilipwa pauni 180,000 (zaidi ya sh. milioni 51) kwa wiki baada ya kumshawishi kocha
Jose Mourinho kuwa yuko fiti.
Nyota huyo anaweza kupata fedha nyingine zaidi kama bonasi.
Ibra awali aliongia mkataba wa mwaka mmoja na huku akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Paris Saint-Germain.
Kabla ya kuumia Aprili alifunga mabao 28 kwa timu ya United katika mashindano yote msimu uliopita, alipata fedha nyingine ziada pauni milioni 2.86 ikiwa na maana kwa jumla aliingiza pauni milioni 21.97 kwa mwaka mmoja.
Ibra sasa atakuwa akivaa jezi namba 10 iliyokuwa ikitumiwa na Wayne Rooney ambaye amerejea katika timu ya Everton.
Wakati huohuo nyota huyo wa Sweden ni amekuwa ni mchezaji pekee wa Ligi Kuu England aliyejumuisha kati ya wachezaji 10 wa Shirikishp la Mpira wa Miguu Ulaya, waliotajwa wakati wa kupanga makundi ya timu zitakazocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Orodha kamili ni kama ifuatavyo;
- Gianluigi Buffon (Juventus)
- Luka Modric (Real Madrid)
- Toni Kroos (Real Madrid)
- Paulo Dybala (Juventus)
- Sergio Ramos (Real Madrid)
- Kylian Mbappe (Monaco)
- Robert Lewandowski (Bayern Munich)
- Zlatan Ibrahimovic (Manchester United)

Comments
Post a Comment