![]() |
| Arsene Wenger |
MCHEZAJI wa zamani Arsenal, Ian Wright amemwomba Arsene Wenger aondoke katika timu ya Arsenal.
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal amesema: “ Tumecheza mechi tatu na tuna matatizo ya ya kupata pointi.
“Ninafikiri kuwa aondoke? ningependa aondoke kwa kuwa siamini kama anaweza kuwahamasisha wachezaji. Ni juu yake na kufikiria kwake.
“Ni ndoto mbaya, atakwenda wapi kutoka hapa? Timu hajacheza kwa Wenger kwa miaka mingi.
![]() |
| Ian Wright |
“Kwanini hatupati wachezaji kucheza kwa ajili yetu? Wenger anawajibika.”
Wright aliichezea Arsenal kati ya mwaka 1991na 1998, michezo 221 na kufunga mabao 128, huku timu nyingi alizochezea ni Greenwich Borough (1985), Crystal Palace (1985–1991), 1998–1999 West Ham United,
1999 Nottingham Forest (kwa mkopo), 1999–2000 Celtic na 2000 Burnley.
Wright pia amedai kuwa Gunners inatakiwa kumuuza
Alexis Sanchez kwa mahasimu wao Manchester City.
Baada ya Arsenal kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool, alisema: “ Ningemuuza Sanchez. kwa nini? Hataki kuwepo pale.''


Comments
Post a Comment