HATIMAYE klabu ya Azam FC imemalizana na Yanga ma kumruhusu mchezaji wake kinda, Gadiel
Michael na sasa atacheza Yanga kukipiga Jangwani.
Mlinzi
huyo alikuwa amebakiza miezi mitano katika mkataba wake na Azam, aliomba
kumwachia ili ajiunge na Yanga na Azam kuwataka viongozi w aYanga kujitokeza
mezani ili kufanya makubaliano.
Baada
ya Yanga kujitokeza na kuzungumza, ililalamika kupiti kwa katibu wake mkuu,
Charles Mkwasa kuwa wametajiwa dau kubwa la kutoka ili kumpata mchezaji huyo,
na kwamba timu hiyo inawabani tofauti na
inavyowaachia wachezaji wake kirahisi wanapotakwia na Simba.
Pia
Gadiel alilalamika kwa Azam FC inambania kwa kutomruhusu kuhamia yanga pamoja
na kwamba ameambia hayumo kwenye mipango ya kocha.
Ofisa
Habari wa Yanga, Jaffar Idd amethibitisha kumalizana na Yanga, kwa kuwaambia
watuo nusu ya dau waliotaka awali na wamefanya hivyo, kwa hiyo Gadiel sasa ni
mali ya Yanga, lakini kenye mkataba wake
kutakuwa na mambo mengine kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili kama atapata
timu nyingine ya kulipwa.

Comments
Post a Comment