![]() |
| Said Fella |
MKURUGENZI wa Diamond Platnumz na mwanzilishi wa kundi la TMK Wanaume Family na Yamoto Band, Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella amesema muziki wa Tanzania umechelewa kunufaisha wasanii nchini kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa mlezi wa kuuongoza.
Mkubwa Fella amesema mbali ya yeye kuwepo kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 15 lakini hajaona ukiwanufaisha wasanii sipokuwa kampuni kupata faida nyingi kupitia kazi za wasanii.
“Muziki wetu umekosa mlezi wa kuuongoza ndiyo maana unakuta aasanii wanaibiwa kazi zao, wananyonywa bila kujua pa kwenda kupeleka malalamiko yao, Unaona watu wanauza kazi za wasanii kiholela”, amesema Mkubwa Fella .
Hata hivyo, Mkubwa Fella ameunga mkono juhudi za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutaka kurekebisha sheria ya masuala ya malipo ya mirabaha kutoka kwenye vyombo vya habari na haki miliki za wasanii ikiwa ni pamoja na kurasimisha tasnia ya hiyo.
Chanzo: Bongo 5

Comments
Post a Comment