LONDON, Uingereza
LIGI ya Mpira wa Miguu England (EFL) inaanza kutumia mfumo mpya wa upigaji penalti ujulikanao kama ABBA katika mashindano yake ya kuanzia msimu huu wa 2017-18.
Mfumo huo uliokwishafanyiwa majaribio na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya( UEFA), msingi wake ni katika mchezo wa tenisi, katika penalti ya kwanza timu zote zitapiga moja moja AB , kisha timu ya pili kuanza kupiga BA kabla ya timu ya kwanza kupiga penalti ya tatu AB na kuendelea tofauti na mfumo wa awali wa timu inayoanza kupiga huendelea hivyo hadi kupata mshindi.
Mtindo huo mpya utafanyiwa majaribio katika msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Ligi, Kombe la EFL na mechi za mchujo za michuano ya Kombe la Ligi itakayoanza Agosti 8-9.
Katika taarifa yake Mtendaji Mkuu wa EFL, Shaun Harvey alisema wanakaribisha ubunifu katika EFL anafurahi kwa kuwa sehemu ya mabadiliko muhimu ya mpira wa miguu.
Alisema mabadiliko hayo yamelenga kuondoa hisia kuwa timu inayoanza kupifa penati katika msumu wa awali ilikuwa haitendewi haki, mfumo mpya mpya umeonekana kufaa kwa kuwa timu zinabadilishana kuanza kupiga penalti.
"Sote tunataka mechi za mpira wa miguu kuamriwa kwa haki na usawa na nina uhakia mfumo mpya itaongeza kitu cha kuvutia katika kuamua mechi katika mashindano yetu kama itatakwia kufanya hivyo.''

Comments
Post a Comment