PAMBANO maarufu kama “The Money Fight” kati ya Floyd Mayweather Jr. vs Conor McGregor linatarajwia kufanyika Agosti 27, mwaka huu, habari njema ni kwamba Dstv kwa kuwajali wateja wake liyalionesha moja kwa moja kupitia chaneli maalum ya muda (pop-up channel) .
kwa mujibu wa taatifa iliyotolewa na Multichoice Tanzania jana, Chaneli hiyo itapatikana katika namba 213 kwa wale wenye kifurushi Premium 184,000 mpaka kifurushi Bomba sh.19, 975 na itaanza Jumamosi hii na kuruka kila siku kuanzia saa 12:00 jioni- 08:00 usiku na kuendelea mpaka usiku wa pambanJumapili, Agosti 27 kabla ya pambano hili kuanza.
Katika chaneli hiyo kutarushwa mapambano mbalimbali ya Mayweather na ziara yake ya Afrika mwaka 2014 pamoja na mbwembe za bondia huyo na jinsi anavyotumia na kujidai na fedha zake.
Kutakuwa na Nguo za thamani, maburungutu ya fedha, magari na lugha za kebehi. Hiyo yote ni kuleta mvuto kwenye pambano hili .
Pambano hilo litarushwa LIVE na Dstv pekee kupitia SS2 Dstv 202 kuanzia kifurushi Premium sh.184,000 tu saa 8:00 usiku-2:30 asubuhi!

Comments
Post a Comment