![]() |
| Diego Costa |
RIO DE JANEIRO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa Chelsea,Diego Costa anajiandaa kuungana na timu yake ya zamani ya
Atletico Madrid pamoja na kwamba timu hiyo ya La Liga ina adhabu ya unayoizuia kusajili hadi Januari mwakani .
Costa hajaichezea Chelsea tangu alipocheza mechi ya fainali ya Kombe la FA Cup Mei, baada ya kudai alitumiwa na ujumbe mfupi wa simu na kocha Antonio Conte unaofahamisha hayumo kwenye mipango yake ya msimu mpya.
Mzaliwa huyo wa Brazil mwenye uraia wa Hispania, aliyejiunga na Chelsea akitokea Atletico mwaka 2014, ameituhumu klabu yake ya Ligi Kuu ya England inafanya kama mhalifu na kusema kuwa yuko tayari kukaa kipindi chake cha miaka miwili iliyobaki katika mkataba akiwa Brazil.
'' Mahari ninakotaka kwenda tayari kumepangwa,"Costa alikaririwa na gazeti la O Globo la Brazil akisema na kuongeza kuwa atalazimka kurejea Atletico Madrid katika msimu ujao.
Ugumu wake kurejea katika Atletico kwa sasa ni kutokana kuendelea kutumikia adhabu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) kutosajili kwa miaka miwili baada ya kuvunja taratibu, Adhabu hiyo inaisha Januari.
Alisema pamoja na kwamba Chelsea haitaki kumwachia, anaamini kuwa suala hilo litaisha kwa sasa wakati akijiandaa kurejea Hispania

Comments
Post a Comment