JOHANNESBURG, Afrika Kusini
ALIYEKUWA mlinda mlango namba moja wa Yanga msimu uliopita Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na timu ya Tuks FC inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini.
Timu hiyo ya iko Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, inasajili wachezaji wenye uwezo ili kupanda Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Dida alikataa kuongeza mkataba Yanga SC ili kutafuta timu nje ili kupata changamoto mpya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu.
Timu nyingine alizozichezea Tanzania ni Simba, Azam FC, Mtibwa Sugar na Yanga huku timu yake ya awali ni Manyema FC, pia amewahi kucheza soka ya kulipwa Oman.

Comments
Post a Comment