![]() |
| Nassibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (wapili kushoto) na wasanii wenzie wanavyoonekana katika Video ya wimbo wa Zilipendwa uliopakuliwa leo. |
Mwandishi wetu
WASANII wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WBC), Diamond Mlatnumz, Harmonize, Rich Mavoko, Maromboso, Queen Darleen, Lavalava na Rayvanny wametoa video ya wimbo wao mpya uitwao Zilipendwa ambao wameimba mambo mbalimbali ya zamani (mambo ya wahenga).
Katika wimbo huo ambao tayari umeanza kupigwa kwenye vituo vya televisheni, redio na kwenye mitandao ya kijamii, wameimba na kufanya ulinganifu wa mambo zamani na sasa sasa wakiangalia kuhusu mapenzi, ugomvi na kutokuelewana kwa watu kulikobakia kama simulizi au zilipendwa.
Wimbo huo umetoka siku moja tu baada ya kutoka wimbo wa msanii Ali Kiba wa Seduce Me (Nitongoze mimi) kitu ambacho kimefanya mashabiki wa pande zote mbili kushindana kwa kupishana kila upande ukiutambia mwingine kuwa wimbo wao ni mzuri.
Katika video Diamond na wasanii wenzie wanaonekana wamekiwa wamevaa mavazi ya zamani na kutumia ala za muziki wamewatumia wasanii waigizaji, kuendana namaneno yanayoimbwa kwenye wimbo huo.
Mapenzi ya zamani zamani wanatu walikuwa wakipelekeana kadi na maua mtu anaridhika , mtu kusema kuwa anampenda mwingine hadi kumwona kwenye glasi ya maji lakini kwa wanwake wa leo wanataka mikakati, ukiwa mzugaji huwapati.
Kuhusu mambo ya zamani waliyoyaimba kama ni zilipendwa ni kama kupiga chabo (kuchungulia ndani kupitia dirishani) na kutaja orodha watu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kuachana ambapo katika kuonesha kuwa hawabagui pia ametajwa Diamond na Wema.
Kuhusu watu waliokuwa na hasama ambao wamebaki kama zilizopengwa wametajwa wengi ikiwemo, Bashite na Gwajima, pia mitindo ya muziki ya zamani kama bolingo, ndombolo, Chipolopolo, Simba wa Morogoro ( Afande Sele), MB Dog wa Latifah, Babu Tale Papa Misifa na hata pati watu hawaendi kibisa imebaki zilipendwa.
Mpira na Pele zilipendwa, Dandu na Nyerere, Asha ngedere, Arous Mabele, Idi Amini, masuala ya kuuza nyumba ili kuweka heshima baa nayo pia zilipendwa.
Mwishoni mwa wimbo huo wanaweza hata masualaya madili yaliyokuwepo enzi za Rais Kikwete sasa enzi za Magufuli imekuwa zilipendwa!


Comments
Post a Comment