![]() |
| asibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz |
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameshirikishwa katika wimbo wa rapa Farid Kubanda, Fid Q wa Fresh Remix ambao umeanza kubamba mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.
Hata hivyo kwenye wimbo huo kuna mashairi ambayo yanaonekana kama yawalenda wabaya wake wanaompinga.
Baadhi ya mashairi ni ,“Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi , kunicompare na Cinderella (wimbo ulioimbwa na Ally Kiba) aaah haiwezi kuwa fresh, Simba kutoka mbuga ya Tandale naona swala wanaforce tuwe salesale viuno vidogo wanataka ya pensi ya Pepe Kale si walitaka kiti nimewapa hadi itanda wakalale.”
![]() |
| Farid Kubanda, Fid Q |
Je ni kijembe kwa kwa akina nani, mashabiki wamekuwa wakitoa tofauti.
Katika wimbo huo Diamond ameimba kwa kurap akianza kwa kusema kuwa kabla ya kuitwa Dangote domo siku hizi anaitwa lips denda, pia amezungumzia kuhusu kuitwa baba Adul kwa sasa wakati yeye ni baba Tiffa na na kusema kuwa mitaani kuna mambo.


Comments
Post a Comment