![]() |
| Ousmane Dembele akipimwa afya katika timu ya Barcelona leo. |
KIUNGO Ousmane Dembele amepimwa afya na kuonekana kuwa fiti kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa pauni milioni 96 (zaidi ya sh. bilioni 277.5) Barcelona.
Nyota huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20, atatarajiwa kutambulishwa kwa mashabiki Jumatatu, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano kwa miamba ya Catalan.
Nyota huyo aliwasili kwenye kituo cha mazoezi cha klabu Ciutat Esportiva leo asubuhi, na kufanyiwa vipimo akihamia timu hiyo akitokea Borussia Dortmund.
Katika video iliyoachiwa na Barcelona kupitia mtandao wake wa twitter, inamwonesha akifanya mazoezi kwenye gym akiwa ni sehemu ya vipimo vya ufiti wa mwili.
Uje ya Uwanja wa Nou Camp, kulikuwa na mashabiki wengi waliofika kutaka kuona wakati akitambulishwa.
Dembele kwa sasa ni ni mchezaji wa pili ghari zaidi akiwa nyuma ya nyota wa Brazil, Neymar aliyesainiwa na PSG kwa ada ya pauni milioni 200 (zaidi ya sh. bilioni 578).
''Nina furaha sana hapa. Imekuwa ni ndoto yangu kila wakati kuwa katika Barcelona, Dembele alisema na kukaririwa na tovuti ya klabu baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano.
Inaaminika dili ya kuleta Dembele Uwanja wa Nou Camp itaigharimu Barcelona hadi kufikia pauni 136 (zaidi ya sh. bilioni 393).
Mshambuliaji huyo ameachwa kwenye kikosi cha ufaransa kwa ajili mechi mbili zijazo za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi na Luxembourg baada ya kutofanya mazoezi katika iliyokuwa timu yake Dortmund wakati akijiandaa kwa uhamisho huo.

Comments
Post a Comment