![]() |
| Philippe Coutinho akiwa na Neymar mazoezini katika timu ya taifa ya Brazil. |
RIO DE JENEIRO, Brazil
KOCHA wa Brazil na rafiki wa muda mrefu wa Philippe Coutinho, Michael Simoni amesema maumivu ya mgongo ya nyota huyo Liverpool yamechangiwa na kuwa na mawazo.
Madaktari amethibitisha kuwa kiungo huyo kwa sasa yuko vizuri na kutoa ruhusa ya kucheza baada ya kuwa na maumivu ya mgongo yaliyofanya awe nje ya uwanja.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amefanya mazoezi na wachezaji wenzie kujiandaa kwa mechi dhidi ya Ecuador ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Coutinho alidai kujisikia maumivu ya mgongo wakati timu yake ilipokuwa katika mashindano ya Kombe la Audi Cup Agosti mosi mwaka huu wakati timu yake ikicheza dhidi ya Bayern Munich na hakufanya mazoezi kuanzia wakati huo.
Pia amekuwa na mafua lakini lakini ameweza kujiunga na nchi yake.
Nyota huyo amekuwa akihusishwa habari za kutakiwa na timu ya Barcelona na Simoni anasema kwa sasa kinachotakiwa ni mazungumzo ya kumtia moyo.
"Coutinho na mimi ni marafiki kianzia miaka mingi. kila wakati nimekuwa nikimpatia matibabu. Anachohitaji ni mtu wa kumpatia maneno ya kumtia moyo.
Daktari mwenzie wa Brazil, Rodrigo Lasmar alisema: " Kuhusu kitabibu, Philippe yuko katika hali nzuri.”
Kocha wa Jurgen Klopp ameweka msimamo wa klabu kwamba Coutinho hatauzwa.
Baada ya timu yake kuibuka an ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Arsenal, Klopp aliiambia Sky Sports kuwa wamiliki wa timu nao hawana nia ya kumuuza.
Coutinho awali aliiomba Liverpool imruhusu aondoke kwenda Nou Camp.
Barca hivi karibuni imemsaini winga wa Dortmund,Ousmane Dembele kwa ada ya pauni milioni138 ili kuziba pengo la Neymar aliyesainiwa na PSG ya Ufaransa kwa ada ya pauni milioni 198.

Comments
Post a Comment