![]() |
| Kocha Jurgen Klopp (kushoto) akizungumza na Philippe Coutinho |
PHILIPPE Coutinho anaonekana kunyoosha mikono kwa kukubali matokeo kuwa imeshindikana kupata uhamisho kuhamia timu ya Barcelona ambayo imeonesha nia ya kumtaka lakini klabu yake ya Liverpool imekataa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, alipeleka barua ya maombi kwa uongozi wa Liverpool kuomba kujiunga na miamba ya Catalan, lakini Liverpool ilikataa maombi yake pamoja na kukataa ofa tatu kutoka timu hiyo.
Barcelona inayonolewa na kocha Ernesto Valverde imekuwa ikisaka mchezaji wa kuziba pengo la Neymar aliyesainiwa kwa Paris Saint-Germain kwa ada ya pauni milioni 198 zaidi ya sh. bilioni 568.
Kwa sasa Barca imekuwa ikisaka mchezaji mwingine baada ya kukataliwa na Liverpool kumsaini Coutinho.
Nyota wa Nice, Jean-Michel Seri anaelezewa uwezekano wake wa kujiunga na timu ya Nou Camp ni asilimia 90 imekamilika, huku kiungo wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele naye akitajwa kukaribia kukamilisha uhamisho.
Coutinho ameachwa katika hali ya sintofahamu na gazeti la Independent limeripoti kuwa yuko tayari kurejea Liverpool na kocha Jurgen Klopp anamkaribisha kwa mikono miwili.
![]() |
| Philippe Coutinho |
Liverpool haijafurahishwa na jinsi Barcelona ilivyochukua hatua ya kulazimisha kumsaini.
Barca inadaiwa kuweka presha kwa familia ya Coutinho nchini Brazil, kitu ambacho kinahisiwa kusababisha kuomba aruhusiwe kuondoka kwa kutumia barua pepe.
Klopp amekuwa akitaka kubakia na Coutinho, aliyefunga mabao14 katika mashindano yote msimu uliopita.
Liverpool imesema Coutinho amekosa mechi mbili za kwanza katika Ligi Kuu England kutokana na kuumia mgongo akiwa fiti atajiunga na timu.
Coutinho Januari mwaka huu alisaini mkataba wa miaka miaka mitano ambao utamweka hapo hadi 2022.


Comments
Post a Comment