![]() |
| Philippe Coutinho |
LONDON, Uingereza
KIUNGO mshambuliaji Philippe Coutinho, ameachwa kwenye kikosi cha Liverpool kitakachocheza mchezo wa mchujo kuwani kufuzu Ligi ya Mabingwa kesho dhidi ya Hoffenheim.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ameiomba klabu yake kumruhusu kuhamia katika mu ya Real Madrid, baada ya klabu yake kukataa dau la euro milioni 100 au pauni milioni 90 ambazo ni zaidi ya sh. milioni 254 kutoka Barcelona.
Jumamosi alikosa mchezo wa kwanza wa ligi Kuu England dhidi ya Watford iliyoishia kwa sare ya mabao 3-3 kutokanana na kuwa majeruhi.
Barca inamtaka Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa timu ya Paris St-Germain kwa uiliyovunja rekodi ya Dunia ya pauni milioni 200.
Coutinho alisaini mkataba mpya wa miaka mitano katika timu ya Liverpool signed Januari mwaka huu, ambao hauna kifungu ya kuvunja mkataba.
Liverpool itaanza kucheza Ligi ya Mabingwa uwanja wa Rhein-Neckar-Arena nchini Ujerumani kabla ya kurudiana Anfiel Jumatano Agosti 23, mwaka huu.
Mshindi atafuzu hatua ya makundi Ligi ya mabingwa.
Kikosi cha Liverpool kilichokwenda ujerumani ni : Alexander-Arnold, Moreno, Lovren, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Mane, Salah, Firmino, Kent, Solanke, Origi, Gomez, Klavan, Flanagan, Robertson, Matip, Grujic, Mignolet, Karius, Ward.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni:
FK Qarabag vs Copenhagen saa 1:00
Apoel Nic vs Slavia Prague saa 3:45
Sporting vs Steaua Buc saa 3:45
Young Boys vs CSKA saa 3:45

Comments
Post a Comment