![]() |
| Antonio Conte (kushoto) na Diego Costa |
KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amemcheka Diego Costa kutokana na madai yake kuwa Chelsea imepanga dau kubwa ili kukwamisha uhamisho wake Stamford Bridge.
Mshambuliaji huyo mwenye uraia wa Hispania lakini ni mzaliwa na Brazil pamoja na kutakiwana timu yake kurejea haraka akiwa huko kwao hajafanya hivyo.
Costa amekwua akifanya mazoezi binafsi ufukweni, awali aliliambia gazeti la
SunSport kwamba anahisi hatendewi haki na klabu hiyo ya London ambayo msimu uliopita aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya pambano la Ligi Kuu kati ya
Chelsea dhidi ya Tottenham katika uweanja wa Wembley kesho, Conte alipoulizwa kuhusu madai ya Costa alisema anaona bora acheke.
“Ninaweza kukwambia wewe kila mmoja katika Chelsea kitu gani kilitokea na yeye msimu uliopita. Sipendi kuendelea kuzungumzia hilo, imeshapita.”
Conte ameviambia vyombo vya habari vya Brazil leo: “Ninaonasha kuijali Atletico ambayo anapenda kuichezea
“Kama Atletico na Chelsea hazijakubaliana na Atletico haifanyi jitihada kubwa, ingekuwa mimi nisingeweza kuendelea kusubiri kuichezea klabu ambayo haifanyi jitihada ya kutoa ofa kubwa katika kujaribu na kunisaini mimi,'' amesema.
Blues aliilipa Atletico pauni milioni 32 kwa kumsaini Costa 2014, amecheza mechi 120 na kufunga mabao 59, ameisaidia kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu na Kombe la Ligi.
Atletico Madrid inadaiwa kuwa tarari kulipwa pauni milioni 30 kwa ajili mchezaji huyo, lakini Chelse inataka kiwango ambacho kinakaribia 50.

Comments
Post a Comment