![]() |
| Diego Costa akiwa na Kocha Antonio Conte. |
LONDON, Uingereza
TIMU ya Chelsea imemwamuru Diego Costa kurejea London haraka iwezekanavyo kutoka kwao Brazil, ili kufanya mazoezi na kuwa fiti ili kurejea kwenye kikosi cha kwanza.
Chelsea mabingwa watetezi, waliopoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England ikiwa nyumbani dhidi ya Barnley kwa kufungwa mabao 3-2, sasa inataka kukaa sawa ili kushinda.
Nyota huyo aliyeongoza kwa ufungaji mabao 20 msimu uliopita, ameamriwa kurejea huku akiwa hana maelewano na kocha Antonio Conte.
Uhusiano kati ya Conte na Costa ulivurugika baada ya kocha kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi katika simu kuwa hayumo kwenye mpango ya timu msimu huu.
Conte amedai uamuzi wa kuachwa kwenye timu ulifanyika Januari mwaka huu wakati alipotaka kwenda kucheza China na aliondolewa kwenye timu na kocha wa viungo Julio Tous baada ya kuzozana naye.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema anataka kurejea Atletico Madrid timu aliyokuwa akiichezea kabla ya kusaini Chelsea, lakini klabu hazijafanya makubaliano.
Wanasheria wa Costa wanataka aachiwe huru kwa sababu mkataba wake umevunjwa kutokana na meseji ya Conte. Chelsea, ambayo inamwona mchezaji huyo thamani yake ni zaidi ya pauni milioni 60 (zaidi ya sh. bilioni 173, haitaki kumpoteza bila ya kupata chochote.
Costa alipewa ruhusa kuchelewa kuripoti kwenye mazoezi ya msimu wakati klabu yake ikifanya mazungumzo na Atletico. Hakujumuishwa kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya ya China na Singapore, lakini uwezekano wa suluhu kupatikana ulitoweka.
Katika mahojiano na Sportsmail yaliyotoka Jumapili, alidai kuwa Chelsea imekuwa ikimfanya kama mhalifu. Alisema kuwa ataendelea kufanya mazoezi kwao kuliko kurejea London katika Uwanja wa Surrey kwa kuwa hawezi kupangwa kucheza.
Chelsea, haina nia ya kumwachia Costa ambaye amebakiza miaka miwili katika mkataba wake unaomfanya kulipwa pauni 180,000 kwa wiki na sasa inaona ina upungufu wa wachezaji.
Swali lililopo kama Costa atarejea ataombana radhi na Conte ambaye naye mkastaba wake unaishwa 2019 na kuendelea kucheza? au Conte anaweza kukataa na kuamua kuondoka.

Comments
Post a Comment