![]() |
| Kylian Hazard |
LONDON, Uingereza
TIMU ya Chelsea imekamilisha dili la kumsaini Kylian Hazard ambaye ni mdogo wa mchezaji wao, Eden na nduguye Thorgan ambao wote walisainiwa katika timu hiyo.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu England imechukua hatua ya kumsaini nyota huyo raia wa Ubelgiji baada ya kuridhika na kiwango chake na kuamini anaweza kusaidia timu yao kuimarika.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefuata nyayo za
kaka yake Eden, alichezea katika timu ya kwanza ya Chelsea na kutwaa nayo makombe mawili ya Ligi ya England na ndugu yake mwingine Thorgan.
Ametua Chelsea akitokea katika timu ya Ujpest ya Hungary , aliyeichezea mechi 42 na sasa atajiunga na kikosi cha maendeleo (akiba) Stamford Bridge.
![]() | ||
Eden Hazard
|



Comments
Post a Comment