LONDON, Uingereza
HUKU ikiwa zimesalia siku 10 kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu England msimu wa 2017/18 kikosi cha kwanza cha Mabingwa watetezi wa Chelsea kina wachezaji 17 tu.
Chelsea hivi karibuni imemuuza mlinzi wake Nemanja Matic kwa mahasimu wao Manchester United, hali inayokiacha kikosi kikiwa na huzuni huku kukiwa na muda mfupi kabla ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa kuanza .
Katika msimu huu Chelsea imemsaini Alvaro Morata kwa ada ya pauni milioni 70.6 (zaidi ya sh. bilioni 209), Tiemoue Bakayoko kwa pauni milioni 40 (zaidi ya sh. bil 118), Antonio Rudiger kwa ada ya pauni milioni 31 zaidi ya sh. bil 91) na Willy Caballero bure
Ikijumuishwa wachezaji iliyowatoa kwa mkopo, Chelsea katika majira haya ya joyo imewaachia wachezaji 26 wakiwemo Nathan Ake, Kurt Zouma, Asmir Begovic, Diego Costa na Matic.
Wadau wa woka wanalaumu kwa kitendo chake cha kukubali kumuuza Matic kwa Manchester United ambao ni hasimu wao.
Kocha Antonio Conte amekuwa akilalamika kwa kutosapotiwa na uongozi kusajili wachezaji wapya wakati timu inakabiliwa na mashindano mbalimbali.
Hata hivyo Chelsea bado iko sokoni ikisaka wachezaji.
Inamwinda Alex Sandro wa Juventus na Antonio Candreva wa Inter wachezaji ambao wamependekezwa na Conte.
Pia inadaiwa kumwinda kiungo wa Leicester, Danny Drinkwater na Alexis Sanches wa Arsenal ambaye leo ameungana na wachezaji wenzie kwenye mazoezi baada ya kutoka katika mapumziko, nyota huyo atajajwa pia kutakiwa na Bayern.

Comments
Post a Comment