![]() |
| Usain Bolt |
USAIN Bolt anaamini kuwa anaweza kupata timu ya kuchezea baada ya kustaafu mchezo wa riadha.
Kwa sasa inawezekana anajiandaa kukubali ofa ya kujiunga na timu ya League One au League Two kuliko timu anayoipenda ya Manchester United.
Boltn (30) ametangaza kujiuzulu kushirikishi mashindano ya riadha baada ya kutwaa medali 19, huku akipata medali ya shaba moja katika mbio za meta 100 za mashindano ya Dunia ya London yalioisha mwishoni mwa wiki.
Nyota huyo wa Jamaica, hakuweza kumaliza mbio za relay 4x100m Jumamosi kutokana na kushikwa na msuli na amesema: “kila wakati zilikuwa nikitaka kucheza soka kwa sababu ni kitu ninachofikiria , nimekuwa mzuri katika hicho.
“Lakini kwa sasa baada kuumia msuli, nimekuwa sina mashaka makubwa sana kuhusu hilo kwa sasa.”
Wakala wa Bolt, Ricky Simms ameliambia gazeti la Daily Star kwam,ba anataka kucheza soka na kwamba wana ofa za klabu nyingi zinazotaka aende kufanya majaribio.
“Sitaki kutaja majina lakini atakwenda Dortmund kwa kuwa CEO (Ofisa Mtendaji Mkuu wa Puma, ambaye ni rafiki yetu yumo kwenye bodi ya Borussia Dortmund. Atakwenda kufanya mazoezi nao .
“Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 anaweza kucheza katika Bundesliga au Premier League? Kiukweli ni hatua ya mbali zaidi.
“Ninafikiri kama atapata muda wa miezi sita au tisa ya kufanya mzopezi na kucheza mechi za kirafiki na timu anaweza kucheza kwa daraja fulani hiyo inaweza kuwa katika League One au League Two.”
Kabla ya hiyo yote, Bolt anatumaini kuwa fiti na kucheza katika mechi kati ya wachezaji nyota wa zamani wa United dhidi ya Barcelona katika Uwanja wa Old Trafford, Septemba 2, mwaka huu.
Katika mechi hiyo ndipo anaweza kuonesha ni kwa kiasi gani mzuri uwanjani.
Simms aliongeza “ anaweza kunipiga mimi kichwani na kusema kuwa anakwenda kucheza katika Ligi ya Mabingwa.
“Lakini sijui kikweli kama amehamasika katika hatua hii ya maisha yake kwenda kufanya mazoezi na wachezaji wa akiba katika siku ya mvua Manchester au Munich au sehemu nyingine kwa kuwa ni mtu mwenye fedha na maisha mazuri. Mnaweza kumuona kupiti katika soka.”
Mchezaji aliyenunuliwa kwa dau kubwa United, Paul Pogba awali alisema kwamba anatarajia Bolt anasaini katika timu ya Jose Mourinho inayosaka ubingwa msimu huu.

Comments
Post a Comment