LONDON, Uingereza
MWANARIADHA nyota mwenye kasi zaidi duniani, Usain Bolt amesema kuwa anasubiri kuitwa na Jose Mourinho ili ajiunge na timu yake anayoipenda ya Manchester United kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Bolt amesema kuwa anatarajia kustaafu mashindano ya riadha baada ya kuisha mashindano ya ya riadha ya mchezo huo yanayotarajia kuanza Agosti 4 hadi 13 mwaka huu jijini London.
Mkimbiaji huyo raia wa Jamaica mwenye umri wa miaka 30 aliyetwaa medali za dhahabu nane katika Olimpiki anajulikana ni shabiki damu wa United amekuwa akimwota Mourinho na Old Trafford baada ya kuachana na riadha.
“Kila mmoja anajua, kila wakati nimekuwa nikizungumzia kuhusu hilo (kucheza) soka, ninasubiri simu kutoka kwa Mourinho,” Bolt alisema akiwa London.
“Ninafikiri anasubiri hadi siku ya mwisho (ya dirisha la uhamisho).”
Mashindano ya Riadha ya Dunia yanatarajiwa kuanza Ijumaa katika Uwanja wa Olimpiki mjini London Ijumaa hii.

Comments
Post a Comment