![]() |
| Usain Bolt akisikitika kwa kutumia muda mwingi katika mbio za meta 100. |
LONDON, Uingereza
BINGWA wa Olimpiki mara nane, Usain Bolt amesema ukimbiaji wake katika mashindano ya kuwa kufuzu nusu fainali mbio za meta100 za mashindano ya Dunia akitumia muda wa sekunde10.07, ulikuwa mbaya haijapata kutokea
Mwanariadha huyo raia wa Jamaica, ambaye ametangaza kustaafu baada ya michuano ya Dunia London, alimshinda, mwingereza James Dasaolu aliyeshika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa sekunde 10.13. lakini hakuanza vizuri mwanzoni.
''Sikuwahi kukutana na hali hii," alisema Bolt na kuongeza kuwa anatakiwa kujiweka sawa
Mmarekani,Justin Gatlin aliyewahi kusimamishwa mara mbili kushiriki riadha kutokana na kutumia dawa za kusisimua misuli, alizomewa wakati akitoka uwanjani.
Waingereza Reece Prescod (10.03) na Chijindu Ujah (10.07) nao wameingia katika tatu bora na kuingia nusu fainali.

Comments
Post a Comment