![]() |
| Bolt akiwa na mpenzi wake, Kasi Bennett |
MWANARIADHA Usain Bolt alifanya starehe usiku kucha kabla ya kukimbia mbio za mwisho za relay 4x100 ambazo alishindwa kumaliza kwa kushikwa na msuli katika mguu wa kushoto.
Rafiki wa karibu aliyekuwa naye katika kujirusha, alisema Bolt alipokuwa klabu usiku alichangamka kwa kucheza na kunywa huku akisalimia kila mtu alikuwa naye karibu, alikuwa kivutio kwa watu waliokuwepo klabu hasa akina dada.
Alisema alimwona akimbusu mdada mmoja alikwepo kwenye klabu hiyo, alijirusha hadi saa 12 asubuhi siku ya mashindano.
Alisema alipokuwa klabu alikuwa akinywa wiski aina ya Hennessy na Wray na Nephew ambzo zote za kijamaica.
Bolt na wenzie walikumbuka maisha ya rafiki yake wa tangu utotoni nchini,Germaine Mason aliyekuwa akishiriki mchezo wa kuruka juu, aliyetwaa medali ya fedha kwa timu ya Uingereza mwaka 2008.
Mason alifariki kwa ajali wakati akiendesha baiskeli, akitoka kwenye hafla nchini jamaica, Aprili mwaka huu.
Akiwa na rafiki zake alishiriki kuchimba kaburi na kubeba jeneza, pia alikwenda kuona sehemu alipopatia ajali.
Bolti anasema kifo cha ghafla cha Mason ikiwa na umri wa kiaka 34 kimemwathiri sana, hakufanya mazoezi ya kutosha kutokana na tukio hilo.
Bolt alisema baada ya mazishi ya rafiki yake hakuweza kufanya mazoezi kwa wiki mbili au mbili na nusu, aliamua kupumzika ili kujiweka sawa.
Alisema mwaka huu umekuwa mgumu kwake, alikuwa na mtazamo wa kutaka kushinda na kuwafurahisha mashabiki wake lakini haikuwa hivyo.
Matumaini ya Bolt kustaafu riadha vizuri kwa ushindi katika mbio za meta 100 yalitowekwa kujikuta akishinda nafasi ya tatu na kupata medali ya shaba akiwa, nyuma ya Mmarekani Justin Gatlin ambaye aliwahi kufungiwa kwa kashfa ya kutumia dawa za kusisimua misuli na Christian Coleman akishika nafasi ya pili.
Bolti amekanusha kwamba kushindwa kwake kufanya vizuri kumechangiwa na kufanya kwake starehe kwenye klabu za usiku London.
Bolt bingwa mara tisa wa medali za dhahabu katika Olimpiki na rafiki zake walionekana katika eneo la VIP la The Box Soho, akiwa na watu maarufu kuna wakati alitembelewa na Prince Harry.

Comments
Post a Comment