![]() |
| Usain Bolt |
TIMU ya mpira wa miguu ya Beira-Mar ya Ureno imempa ofa mwanariadha alikuwa mwenye kasi zaidi duniani ambaye ametangaza kustaafu mchezo huo, Usain Bolt ambaye amesema atataka kuendeleza kupaji chake cha kucheza soka baada ya kuacha na kufukuza upepo, ajiunge nayo lakini atakuwa akilipwa baga na bia.
Hata hivyo Bolt kwa sasa ni majeruhi, aliumia msulu wakati akikimbia mbio za relay (kupokezana vijiti 4x100m) kitu ambacho inawezekana kikafanya iwe ngumu kusajiliwa na timu yoyote wakati huu ambapo dirisha la usajili linaelekea mwishoni.
Bolt alitumia mtanda wa Tweeter alihamisi kwa kusema kuwa amechanika nyama za paja kitu ambacho kilisababisha ashindwe kumalizia mbio, atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu ili kupata matibabu na kupona.
Beira-Mar awali ilimpa ofa Bolti kujiunga nayo kupitia ukurasa wao wa Facebook.
“Usain Bolt, njoo na utimize ndoto yako,”Waliiandika. “ Njoo na ucheze soka kwa Beira-Mar!”
Pamoja na kwamba atakuwa nje ya uwanja na kuonwa na mashabiki wake wakati akitibiwa atakuwa akilipwa kwa kuonekana katika matukio mbalimbali.
Umajeruhi huo umefanya ndoto yake ya kucheza mpira wa miguu mpira wa miguu wa kulipwa.
Nyota huyo alisema anapenda sana simu moja asajiliwe na kuichezea Manchester United timu ambayo anaipenda.

Comments
Post a Comment